Safiri kwenda nyumbani kwa bei yako — Sheria na Masharti ya Promosheni


1. Mratibu wa Promosheni hii ni kampuni ya Havas Media Kenya Limited. Huduma ya inDrive ndiyo Mwandalizi.

2. Tarahe 23 mpaka 27 Disemba 2022, huduma ya inDrive itawapa watu 700 wa kwanza punguzo la bei kwenye safari ( Mlimani City Shopping Mall - 70 kwa siku, na kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichoko Mbezi - 70 kwa siku), katika kila siku ya promosheni hii, wasafiri watapunguziwa kiasi cha TZS 7000 kwenye usafiri ambao wataagiza kupitia ap ya inDrive kutoka Mlimani City Shopping Mall, au Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichoko Mbezi jijini Dar Es Salaam, Tanzania hadi mwisho wa safari zao.

3. Ofa hii itatumika mnamo Disemba 23 hadi 27 mwaka wa 2022 kwa ajili ya safari zinazoanzia Mlimani City Shopping Mall, au Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichoko Mbezi jijini Dar Es Salaam, Tanzania kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa moja jioni na tarehe 25 Disemba2022 muda wa promosheni ni kuanzia saa sita kamili mchana mpaka saa moja kamili usiku. Mchakato wa malipo utaendeshwa na timu ya wasaidizi wa Havas Media Kenya Limited watakaokuwa katika Mlimani City Shopping Mall na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichoko Mbezi jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

4. Ofa hii itatumika tu kwa safari za kutoka Mlimani City Shopping Mall, au Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli kilichoko Mbezi hadi mwisho wa safari na ni iwapo safari hiyo itaagizwa kupitia ap ya inDrive.

5. Ikiwa gharama ya safari itakuwa chini ya thamani ya punguzo, kiasi kilichosalia hakiwezi kutumia kulipia safari ya baadaye. Ikiwa gharama ya safari itakuwa zaidi ya thamani ya punguzo, aliyeagiza safari atahitajika kulipa kiasi kilichosalia kwa dereva wa inDrive.

6. Ofa hii haiwezi kuhamishwa, kufanyizwa upya, au kuuzwa. Ofa hii haitumiki kulipia ada za ziada, ada za barabarani au bashishi.

7. Huduma ya inDrive, kwa hiari yake, inaweza kubadilisha au kuondoa kikamili au sehemu ya ofa hii wakati wowote na bila kutoa taarifa mapema.

8. Washiriki wowote, katika hali yoyote ile, wanaondolea inDrive lawama, pamoja na mawakala wa matangazo, washauri, mawakala waliopendekezwa, mashirikia yanayouzia inDrive bidhaa na huduma, washirika na/au makampuni yanayohusishwa na inDrive dhidi ya madai ya aina yoyote yanayotokana na kushiriki kwao kwa namna yoyote ile katika mpango huu wa promosheni (ikiwa ni pamoja na, kutokana na kutenda au kukosa kutenda jambo fulani, ikiwa ni kutokana na utepetevu, kutoa taarifa za uongo, au kufanya kosa au jambo lingine lolote litakalofanywa na Waandalizi na/au linalohusiana na matumizi ya vocha ya punguzo).

9. Baada ya washiriki kukubali ofa ya promosheni hii, wanawajibika kikamilifu kulipia gharama zote zinazohusiana na punguzo hili, ikiwa ni pamoja na, bali sio tu, ushuru wowote wa serikali za mitaa na taifa.